Tembo alitaabika sana kwa sababu ya ukubwa wa pua lake. Alikuwa anataka kujua siri ya mjusi iliyomwezesha kutembea kwa ukuta bila kuanguka. Aliona kama muujiza. Tembo aliona hangeweza kujificha kutoka kwa adui kwa sababu ya mwili wake.
Mjusi akamwomba tembo ammiminie maji badala ya kuingia majini. Ndiposa akamwelezea siri yake.
Hapo zamani za kale mababu wa mjusi walikuwa na miili mikubwa kuliko wanyama wote.