Kulikuwa na tatizo kubwa. Paka Samantha alikuwa anakula panya wengi na alikuwa hajashiba vya kutosha. Panya hao waliitisha mkutano na kuamua kuwa watasuluhisha tatizo hilo.
‘Sisi ni wengi na paka ni mmoja tu. Tunaweza kumkamata huyu paka.’ ,mmoja wa panya akasema.
‘Paka ni mjanja sana na mvumilivu sana. Anajua kuwa sisi panya ni walafi sana na hatuna subira ikifika wakati wa kula chakula. Sisi mara mingi tunapoteza fahamu tunapoona chakula. Paka anajua tabia yetu.’, panya wa hekima akasema.
‘Kwahivyo tufanyeje?’’, panya mmoja akauliza.
‘Kwanza inabidi tujifunze kusubiri ’, akasema jenerali wa panya. ‘Tunapojifunza jinsi ya kungoja na kutulia pahali pa moja tutaweza kunasa paka na kumfunza adabu na basi tutakuwa na nafasi nzuri ya kumfunga paka kengele.’