Skip to content
Takajua
Takajua

Uko hapa?  Soma stori nifuate kwenye FB, twitter na unione youtube.

 

Skip to content
takajua

takajua

Habari gani?

Youtube
  • Kamusi Yangu
  • Tuwasiliane
  • Home
  • 2022
  • Novemba
  • 24
  • Supu moto yamtia flamingo woga wa maji
flamingo sufuria ndani

Supu moto yamtia flamingo woga wa maji

takajuaNovemba 24, 2022Novemba 25, 2022

Samaki na flamingo walipenda sana kuogelea ziwani. Kwa sababu hii wakawa marafiki. Kila walipokutana katika ziwa majisafi flamingo alimpa samaki uhondo za kule alikokuwa na yale aliyoyaona. Samaki naye alimhadithia flamingo matukio ya kule ndani majini.

Wakati mwingine flamingo alimhadithia samaki kuhusu vyakula vitamu alivyokuwa akila milimani na ndio sababu alikuwa na afya nzuri. Alisema pia hewa safi aliyokuwa akipumua kule angani ilikuwa inasafisha mwili wake kutoka makali ya maji ya ziwa majisafi.

Samaki alisikia haya yote na alitamani sana kuona na kula vitamu lakini haingewezekana kwa sababu hakuwa na mabawa kama flamingo.

Siku moja flamingo akamwelezea samaki kuwa kuna karamu kubwa ilyokuwa imeandaliwa kule milimani na kwamba wote wamealikwa. Samaki akamwomba flamingo amletee vitamu ili aweze pia kuonja. Flamingo akakubali na siku iliyofuata akajiandaa na kuelekea milimani kwa karamu.

Akiwa angani akaona sufuria kubwa iliyokuwa na harufu nzuri ya chakula kitamu. ‘Duh’ , alisema flamingo ‘Sufuria kubwa jameni. Chakula imo ndani yake kitamu kinavutia. Mle ndani lazima nitaingia.’

Ghafla bin vu akashuka kutoka angani kwa kasi huku macho yakiwa yamelenga sufuria.

Asijue kwamba sufuria ilikuwa na supu moto flamingo akaingia ndani kwa miguu yake yote miwili kama kuogelea ndani ya maji. Alipiga mayowe na kutoka mbio huku akidondonkwa na machozi ya uchungu. Hadi sasa anapoingia majini mguu wake mmoja huinua kama kupima hali joto kabla ya kuingiza yote.

flamingo, machozi, mayowe, samaki

Urambazaji wa chapisho

Previous: Watu kuvutiwa na ngoma ya chui
Next: Ngamia asakata rumba uwanjani

Tazama pia

mzee panya na mbuzi shambani

Wale wanaouza matunda ya uchumi uliokumbwa na matatizo

Septemba 14, 2023 takajua
vurugu ya akili bandia

Tisho Akili Bandia kuvuruga maisha ya binadamu

Juni 2, 2023Juni 9, 2023 takajua
samaki apoteza machozi baharini

Samaki akilia machozi yabaki baharini

Mei 5, 2023Mei 5, 2023 takajua

  • GANI NDIO SAHIHI?
  • JE, UNAJUA?
  • KITENDAWILI
  • KWA NINI?
  • METHALI
  • NI UKWELI?
  • SIKU MOJA
Haki zote zimehifadhiwa | Theme: BlockWP by Candid Themes.
Habari gani? Takajua ©2022