Tumbili walishangaa kuona miti ikipungua. Jua likiwaka liliwapiga bila huruma kwa sababu hapakuwa na kivuli.
Adui zao waliwaona kwa urahisi kwa sababu hapakuwa na mahali pa kujificha.
Wakafanya mkutano na kumtuma mfalme wao apate kujua mahali miti yao inapotelea.