Skip to content
Takajua
Takajua

Uko hapa?  Soma stori nifuate kwenye FB, twitter na unione youtube.

 

Skip to content
takajua

takajua

Habari gani?

Youtube
  • Kamusi Yangu
  • Tuwasiliane
  • Home
  • 2023
  • Mei
  • 5
  • Samaki akilia machozi yabaki baharini
samaki apoteza machozi baharini

Samaki akilia machozi yabaki baharini

takajuaMei 5, 2023Mei 5, 2023

Mzee Kasumba hakulala hiyo siku alipoambiwa atafute machozi ya samaki.

“Nitajua aje ni machozi? Nitajua kama ni maji?”, mzee Kasumba akaijiuliza.

Kukamata machozi ya samaki haikuwa rahisi , kwa sababu samaki walikuwa ndani ya maji kila wakati, pamoja na machozi yanahitaji kuhifadhiwa vizuri ikiwa yatapatikana. Mradi huu unahitaji subira sana.

Mzee Kasumba alijaribu mbinu nyingi kutega samaki na jinsi ya kuhifadhi machozi ipasavyo mara tu alipowakamata.

“Katika majaribio mengi nilinasa maji chumvi bila kujua. “

Siku moja mzee Kasumba alipata kuvua samaki wengi lakini hakupata hata tone moja la machozi.

“Mzee unatatizo gani?”, samaki mmoja akauliza.

Mzee Kasumba alikuwa akilia aligutuka na kushindwa kutamka.

“Usiwe na hofu niambie unachotaka”, samaki aliendelea kusema.

Mzee aliporudiwa na fahamu alijibu kuwa alikuwa akitafuta machozi ya samaki.

Samaki kusikia hayo alishangaa na kumuliza sababu ya kutaka machozi ya samaki.

Mzee Kasumba akamweleza kuwa angelipata utajiri ikiwa angelipata machozi yake.

“Nirudishe majini basi”, samaki akamjibu “Nitakueleza jinsi utakavyopata machozi yangu.” , samaki akaendelea.

Bila kufikiria mara mbili mzee Kasumba akatupa yule samaki majini na kusubiri jibu.

Muda uliyoyoma bila jibu na kwa hasira akatupa takataka ndani ya maji ili samaki arudi kutoka majini.

Hadi leo maji baharini imejaa takataka kwa sababu hakuna aliyewahi kuona machozi ya samaki.

bahari, gutuka, machozi, muda, takataka

Urambazaji wa chapisho

Previous: Moja mbili tatu wanajificha nisiwapate
Next: Simba tisa waingia boma ya mbuzi kumi

Tazama pia

flamingo sufuria ndani

Supu moto yamtia flamingo woga wa maji

Novemba 24, 2022Novemba 25, 2022 takajua
ngoma ya chui

Watu kuvutiwa na ngoma ya chui

Novemba 19, 2022Novemba 19, 2022 takajua
garindege bila mafuta

Garindege apotea njia baada ya kumtoroka ndege

Oktoba 31, 2022Oktoba 31, 2022 takajua

  • GANI NDIO SAHIHI?
  • JE, UNAJUA?
  • KITENDAWILI
  • KWA NINI?
  • METHALI
  • NI UKWELI?
  • SIKU MOJA
Haki zote zimehifadhiwa | Theme: BlockWP by Candid Themes.
Habari gani? Takajua ©2022