Kamata mdudu ulimi wa chura

Alipokuwa akipumzika na kujistarehesha akaona wadudu waliovutiwa na ile maua wakimkaribia wasijue kwamba anatamani kula wadudu.

Chura aliomba aweze kupata chakula ili apate nguvu. Chura alipotazama mtoni akaona maua mengi ya kupendeza, lakini aliogopa sana mwendo kasi wa maji kwamba ikiwa angejaribu kuingia, angezama.

Wazo likamjia aruke hadi afikie ua moja apate kujistarehesha juu yake. Moja kwa moja na bidii yake yote akanyanyua miguu yake na kuruka na kutua juu ya ua moja mtoni. Alifurahi sana alipofaulu hata kama alikuwa hana nguvu . Alipokuwa akipumzika na kujistarehesha akaona wadudu waliovutiwa na ile maua wakimkaribia wasijue kwamba anatamani kula wadudu.

Bila kusita akiwa ametulia akafungua kinywa chake na kuwanasa wale wadudu. Aliendelea hivo hadi akashiba. Ombi lake lilikuwa limesikiwa.