D – J
D
Dada
Ndugu wa kike
Dawa
Kitu kinachotumika kutatua shida fulani kama ugonjwa
Dadisi
Uliza kwa kupeleleza
Dafrau
Kugongana kwa vitu viwili
Daftari
Kitabu kinachotumika kuweka hesabu ya vitu
Dai
Itisha kitu kilicho chako
Daima
Kutokea bila kukoma
Dakika
Sehemu moja ya saa moja. Kwa kifupi sekunde sitini ni saa moja.
Daktari
Mwenye maarifa ya matibabu
Dalili
Alama au ishara ya kitu kufanyika au kufanywa
Daraja
Kitu kilichotengezwa kwa chuma au mawe au miti kuvukisha watu au magari
Darasa
Kikundi cha wanafunzi wanaopata funzo moja
Demokrasia
Mtindo wa kutawala
Dereva
Mtu anayeendesha gari ardhini
Dhahabu
Aina ya madini iliyo na gharama Zaidi hutumiwa pia kama sarafu
Dhambi
Kosa
Dhiki
Tia kwenye shida
Dhoofika
Afya kuwa hali mbaya
Dhulumu
Taabisha au tesa
Dira
Kifaa kinachotumiwa na wasafiri kuwaelekeza
Doa
Alama tofauti na zilizo kando
Dondoka
Kuondoka kwa mtu pahali palipo juu
Dua
Ombi linaloombwa Mungu
Duka
Aina ya mjengo panapofanyiwa biashara
Dunia
Bara zote pamoja na bahari zinazozizunguka
Duaradufu
Yai iko na umbo la duaradufu
Dumu
Endelea kuishi bila kuzembea
Dume
Mnyama wa kiume
Duara
mchoro wa mviringo
Duni
Isiyo na dhamani kubwa
Duma
Mnyama kama chui lakini mwenda kasi kuliko wanyama wote
E
Ebu
Samahani kwa nguvu
Egesha
Weka gari mahali maalum wakti imesimama
Enda
Kuelekea mahali fulani
Elekea
Enda upande fulani
Eleza
Toa habari au ufafanuzi wa jambo
Elimisha
Patia mtu mafundisho kama masomo
Elimu
Masomo yanayotolewa shuleni
Endesha
Ongoza au elekeza chomba cha kusafiria
Enea
Sambaa kila mahali
Embe
Aina la tunda lililo na kokwa moja kubwa
Enyewe
Peke yake
Ekundu
Rangi ya damu
Enzi
Muda au kipindi cha utawala
Epuka
Kufaulu kutoambukizwa au kushikwa
Eupe
Kinyume na nyeusi au rangi ya theluji
Eusi
Rangi ya kaa
Ezeka
Weka juu
F
Fadhili
Toa usaidizi wakati wa shida
Fafanua
Eleza waziwazi
Fagia
Kufuta au kuondoa kabisa
Fahali
Dume la mnyama
Fahamu
Uwezo wa kujua
Fahari
Enye sifa nzuri
Faida
Kitu au jambo lenye maana
Familia
Mama, Baba na watoto
Fanaka
Baraka au ushindi
Fanana
Kuwa na sura au maumbile sawa
Fanikiwa
Shinda au pata fanaka
Fanya
Tenda kitendo Fulani
Farasi
Mnyama aliye mkubwa wa jamii ya punda
Fariji
Kumtuliza mtu anapopatwa na msiba au mkosi
Fariki
Tokwa au poteza na uhai
Fasiri
Toa maana ya jambo lisilo wazi.
Faulu
Shinda au kufuzu mtihani au zoezi
Fedha
Pesa
Fedheha
Aibu
Feki
Bandia
Ficha
Weka kitu mahali ambapo hapajulikani
Fika
wakati Fulani kutimia
Fikiri
Tumia akili kupata suluhu au kulitatua
Finya
Shika au bana
Fisi
Mnyama wa porini ambaye hupiga kelele kama nduru
Foleni
Mlolongo
Fuata
Andama nyuma
Fuja
Fufuka
Toka kwenye mauti
Fujo
Hali ya kukosa utulivu
Fundi
Mtu mwenye maarifa maalum ya kutengeneza au kurekebisha
Funika
Weka juu ya kinachoonekana kwa kuziba
Funga
Kuweka kizuizi
Futa
Toa kilichowekwa au kuandikwa
Fyeka
Kata nyasi au miti kwa kupunguza
G
Gaagaa
Geukageuka pale ulipolala. Garagara
Gaidi
Mwizi wa kutatiza watu
Ganga
Rekebisha kitu kilichoharibika
Gari
Chombo cha kusafiria barabarani chenye magurudumu Zaidi ya tatu
Gawa
Tenga katika sehemu mbalimbali
Gazeti
Karatasi yalichapishwa ili kuarifu
Gereza
Mahali wanapozuiliwa mahabusu
Ghafla
Bila kutazamia au kutarajia
Ghorofa
Nyumba lililo na nyumba juu ya nyingine
Giza
Kutokuwa na mwangaza
Ghasia
Fujo
Goigoi
Mtu mlegevu au mvivu
Gundua
Fichua jambo
H
Haba
Chache, kidogo
Habari
Ujumbe
Hadaa
Danganya
Hadithi
Habari za kubuni
Hai
Enye kuishi
Haidhuru
Tamko la kuonyesha kutojali
Halafu
Baada ya au kisha
Halisi
Inayokubalika
Hakimu
Halali
Hapana
Neno la kukataza
Haraka
Upesi
Haribu
Potosha au kuridisha maendeleo nyuma
Hatari
Hali ya kukosekana salama
Hasira
Ghadhabu
Hekima
Akili ya ndani au busara
Historia
Hesabu
Hukumu
Holela
I
Ibada
Idhaa
Matangazo ya redio
Ibuka
Tokea bila kutarajiwa
Idadi
Wingi au uchache wa kitu
Idhini
Ruhusa
Ikulu
Makao rasmi ya rais
Iva
Chakula au tunda kuwa tayari kula
Injini
Mtambo wa kutia nguvu au nishati
Ingia
Kuelekea ndani ya kitu kupitia mlango kwa mfano
Inspekta
Afisa wa polisi
Inua
Weka kitu juu au nyanyua
Ishara
Alama ya kitu fulani
Insha
Simulizi kwa mtindo wa nathari
Ishi
kaa
Itikia
kubali
Inchi
Kipimo cha urefu sawa na sentimita 2.5
Ita
Kumtaka mtu aje kwake
Ishirini
Nambari kumi mara mbili
J
jabali
mwamba mkubwa
jadili
ongea au kuwa na mazungumzo kuhusu jambo Fulani kwa mapana
jahazi
chombo cha baharini
jamaa
watu wa damu au ukoo mmoja
jambazi
mwizi atumiaye silaha
jamhuri
nchi iliyo huru
jeshi
jumla ya askari wa kulinda taifa
jino
kifupa kilicho mdomoni kitumiwacho kusiaga au kukata chakula
jitu
mtu mkubwa
jogoo
kuku dume
jiji
mji mkubwa